JINSI YAKUPIKA KEKI YA ZABIBU KAVU
Tengeneza keki ya zabibu
kavu kisha ongezea ladha mbali mbali kutokana na upendavyo fata maelekezo hapo
chini
Mahitaji:
240gram zabibu kavu
240garm maziwa ya maji
240garm siagi (butter)
½ chumvi kijiko kidogo
cha chai
240gram sukari
240gram korosho au
walnuts au karanga chochote ulichonacho
500gram unga wa ngano
1 kijiko kidogo cha chai
baking soda (Baking powder)
2 mayai
JINSI YAKUTENGENEZA
Washa oveni yako katika
joto 325 degree F (165 degree C) kisha kipake chombo chako siagi utakacho tumia
kuokea keki yako.
Chukua bakuli changanya
unga wa ngano, zabibu na baking soda kasha weka pembeni.
Chukua bakuli nyingine
weka siagi na sukari ndani kisha piga mapaka ichanyanyike vizuri na kua laini
kabisa kisha vunjia mayai ndani piga paka mchanganyiko wako uwe laini kabisa.
Kisha chukka
mchanganyiko wa unga mimina kwenye mchanganyiko wa mayai changanya pole pole
mpaka upate mchanganyiko mzito wa wastani kama itakua nzito sana ongeza maziwa
kama itakua nyepesi sana ongeza unga.
No comments:
Post a Comment